6.4 C
New York

Madrid yabisha hodi UEFA ‘ishu’ ya Vinicius

Published:

MADRID, Hispania

Mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilisimama kwa dakika 10 baada ya Vinicius kumlalamikia mwamuzi kuwa mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni, amemwita nyani.

Prestianni alionekana akizungumza huku akiwa ameziba mdomo wakati Vinicius akishangilia bao mbele ya mashabiki wa Benfica.

Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) lilieleza kuwa litafanya uchunguzi kubaini undani wa tukio hilo na kile alichokisema kiungo huyo.

Vinicius amekuwa na mkosi wa kufanyiwa matukio ya ubaguzi wa rangi tangu Mbrazil huyo aliposajiliwa na Madrid mwaka 2018.

Kwa upande wao, Benfica wameendelea kumkingia kifua Prestianni wakidai kuwa kinachoendelea ni kampeni chafu dhidi ya klabu hiyo ya Ureno.

Wakati huo huo, kocha wa Benfica, Jose Mourinho, ambaye pia amewahi kuinoa Madrid, amemlaumu Vinicius akisema lilikuwa ni kosa kushangilia mbele ya mashabiki wa upinzani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img