9 C
New York

Waziri wa Nishati adakwa akijaribu kutoroka

Published:

KYIV, Ukraine

ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Nishati wa Ukraine, German Galushchenko, anashikiliwa na vyombo vya dola baada ya jaribio lake la kutorokea ughaibuni kugonga mwamba.

Galushchenko alilazimishwa kuachia ngazi mwaka jana baada ya kashfa nyingi za rushwa zilizokuwa zinamkabili.

Ndiyo, alikuwa miongoni mwa vigogo kadhaa wa Serikali waliotajwa wakati huo kujichotea Dola za Marekani milioni 100 zilizokuwa kwenye miradi ya maendeleo.

Skendo hiyo ilitishia kuung’oa utawala wa Rais Volodymyr Zelensky, kabla ya nchi hiyo kuvamiwa rasmi na Urusi.

Ni kutokana na presha ya kashifa hiyo, aliyekuwa mshauri wa Rais Zelensky, Andriy Yermak, alitangaza kujiuzulu.

Sasa, Galushchenko amekamatwa baada ya kukutwa kwenye treni iliyokuwa ikiondoka nchini Ukraine, ingawa haijafahamika alikotaka kwenda.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img