13.1 C
New York

Raia wa Syria hawataki kuondoka Ujerumani

Published:

MUNICH, Ujerumani

LICHA ya jitihada za Serikali ya Ujerumani, raia wengi wa Syria hawataki kuondoka nchini humo ili kurejea makwao.

Raia wa Syria takribani 6,000 waliomba mamlaka za Ujerumani kuwarejesha nchini kwao mwaka 2025, lakini bado wengi wao hawataki kurudi nyumbani.

Ujerumani imeendelea kuwashawishi raia hao kurudi Syria, ambako wanagoma kutokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea.

Katika jitihada za kuwashawishi, Serikali ya Ujerumani imekuwa ikifadhili gharama za usafiri, achilia mbali kiasi cha fedha kwa ajili ya kujikimu.

Kupitia Ofisi ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Ujerumani (BAMF), raia wa Syria 16,576 waliofanya maombi ya hiyari wameweza kurejea nchini kwao.

“Jumla ya watu 16,576 wamewezeshwa kurudi katika nchi yao ya asili (Syria) au katika nchi za dunia ya tatu zilizokubali kuwapokea,” imeeleza taarifa ya BAMF.

“Kwa mwaka 2025, wengi kati ya walioondoka kwa hiyari walirudi katika nchi zao za asili za Uturuki, Syria, Urusi, Georgia na Iraq.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img