4.3 C
New York

Simu, ‘laptop’ zinavyohatarisha maisha yako

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

HIVI unafahamu kuwa betri zinazotumika katika simu au kompyuta-mpakato (laptop), ambazo kwa lugha ya Kiingereza hufahamika kwa jina la ‘rechargeable batteries’, ni hatari kwako?

Ndiyo, kwa mujibu wa tafiti, betri hizo ni chanzo cha matukio zaidi ya 15,00 ya moto wa majumbani kila mwaka.

Wataalamu wanasema betri hizo huwa na moto mwingi kwenye eneo dogo, hivyo hulazimika kupita taratibu.

Endapo betri itakumbana na mazingira ya kuilazimisha kupitisha nishati kwa nguvu, ndipo hatari ya mlipuko inapotokea.

Ni katika mazingira yapi? Kuweka betri katika mazingira yenye unyevu, ‘kuchaji’ muda mrefu au mara kwa mara, kutumia ‘chaja’ tofauti na kuweka juani, ni baadhi tu ya mazingira rafiki kwa mlipuko kutokea.

Wakati huo huo, si kila kampuni ya utengenezaji wa simu au kompyuta-mpakato inazingatia usalama wa mtumiaji.

Wakati mwingine, tatizo la betri kulipuka na kusababisha moto linaweza kuwa limeanzia kwa kampuni, mathalan uunganishaji wa vifaa haukuzingatia ubora.

Nini unapaswa kufanya? Hakikisha unanunua simu au kompyuta-mpakato kutoka katika kampuni inayosifika kwa kuzingatia ubora, badala ya kusukumwa na mihemko ya ushawishi wa marafiki au matangazo ya mitandaoni.

Pili, unashauriwa kuacha kutumia simu au kompyuta-mpakato pindi unapogundua kuwa betri lake linachemsha (joto lisilo la kawaida). Achana nayo, maana inaweza kuashiria mlipuko wa siku chache zijazo.

Katika hilo, inashauriwa kuweka utaratibu wa kuwapelekea wataalamu wakusaidie kukagua ufanisi wa vifaa vya simu au kompyuta-mpakato yako walau kila baada ya mwaka mmoja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img