LONDON, Uingereza
HABARI mbaya kwa mashabiki wa Arsenal ni kwamba kiungo wao raia wa Hispania, Mikel Merino, hatarejea dimbani hadi msimu ujao.
Moreno amekosekana katika mechi nne za hivi karibuni, ikiwamo iliyopita ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sunderland iliyochezwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Nyota huyo ambaye amecheza mara 32 msimu huu, atafanyiwa upasuaji wa mguu leo Februari 9, 2026, hivyo atakosekana hadi msimu unaofuata.
Kocha Mikel Arteta amekuwa akimtumia Merino katika eneo la mshambuliaji wa kati kutokana na kusuasua kwa kiwango cha Viktor Gyokeres.
Kabla ya majeraha, tayari mchezaji huyo alishapachika mabao sita na kutoa ‘asisti’ tatu katika michezo 32 aliyoshuka dimbani.


