13.9 C
New York

Mbappe awekwa ‘levo’ za Ronaldo

Published:

MADRID, Hispania

KWA mujibu wa kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa, Kylian Mbappe ana mchango mkubwa kikosini, kama alivyokuwa Cristiano Ronaldo miaka kadhaa iliyopita.

Alberoa ametoa maoni hayo baada ya Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Valencia katika mchezo wa La Liga uliochezwa jana Februari 8, 2026.

Katika mchezo huo, Madrid ilipata mabao yake kupitia kwa Mbappe na Alvaro Carreras. “Ni jambo zuri kuona tunaendelea kuimarika,” amesema kocha huyo.

Akimzungumzia Mbappe, Alberoa amesema Mfaransa huyo anaweza kuyazidi mafanikio aliyopata Ronaldo endapo ataendelea kucheza kwa kiwango bora.

“Tuna bahati kuwa na mchezaji wa aina yake. Ni mchezaji bora duniani kwa sasa. Nimewahi kusema Ronaldo ni kama kiumbe wa ajabu, lakini Mbappe anafuata nyayo hizo pia,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img