10.7 C
New York

Staa mpya Liverpool apata majanga

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

NYOTA mpya wa Liverpool, Jeremy Jacquet, amepata majeraha ya bega akiwa uwanjani kuitumikia Rennes ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 20, amesajiliwa na Liverpool kwa Pauni milioni 60 lakini atajiunga nao mwishoni mwa msimu huu.

Katika mchezo dhidi ya Lens, ambao Rennes walitandikwa mabao 3-1, Jacquet aliumia kipindi cha kwanza. Nyota mwenzake wa Rennes, Abdelhamid Ait Boudlal, naye alipata maumivu ya misuli.

Hatua ya Liverpool kuhamia kwa Jacquet ilikuja baada ya klabu hiyo kukwama katika mpango wake wa kumchukua Marc Guehi aliyetua Manchester City akitokea Crystal Palace.

Chelsea nao walijaribu bila mafanikio kumsajili Jacquet, ambaye ameshacheza mechi tano akiwa na U-21 ya England.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot, ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo na amekuwa akimtaja kuwa ni kipaji kikubwa kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img