10.7 C
New York

Chisora v Wilder: Vita ya karne ngumi za uzito wa juu duniani

Published:

LONDON, Uingereza

NI rasmi sasa Derek Chisora na Deontay Wilder watavaana, huku pambano hilo la ngumi za uzito wa juu duniani likitarajiwa kupigwa Aprili, 2026 katika Ukumbi wa 02 Arena jijini London.

Hilo litakuwa pambano la 50 kwa Chisora mwenye umri wa miaka 42, kama ilivyo kwa Wilder (40).

Awali, Chisora raia wa Uingereza aliweka wazi kuwa atastaafu baada ya pambano lake la 50. Hivyo, huenda akaachana na ndondi Aprili, 2026.

Miaka 13 iliyopita, wawili hao walipaswa kuzipiga lakini Wilder alilazimika kujitoa baada ya kukabiliwa na kesi ya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya mpenzi wake.

Chisora, kwa upande wake, ametoka kushinda mapambano matatu mfululizo, ikiwamo ushindi wa pointi mara mbili mbele ya Joe Joyce na Otto Wallin.

Wilder amewahi kuwa miongoni mwa mabondia hatari wa uzito wa juu alipotwaa mkanda wa WBC mwaka 2020 baada ya kushinda mapambano 40 mfululizo.

Baada ya sare dhidi ya Tyson Furry mwaka 2018, Wilder alipoteza mapambano mawili mfululizo mbele ya mpinzani wake huyo. Hiyo ilikuwa mwaka 2020 na 2021.

Baada ya ukimya wa takribani mwaka mmoja, Wilder alirejea ulingoni Juni, 2025, ambapo alipata ushindi wa ‘KO’ ya raundi ya saba dhidi ya bondia asiye na jina kubwa, Tyrrell Anthony Herndon.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img