11.2 C
New York

Simba maji ya shingo CAF, yaambulia sare kwa Esperance

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

LICHA ya kuongoza kwa mabao 2-0, Simba imejikuta ikiambulia pointi moja baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Esperance, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo ni ya hatua ya Kundi D msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika, imechezwa leo Februari Mosi, 2026.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, Simba ilikuwa mbele kwa mabao ya beki wa pembeni, Shomari Kapombe, na kiungo Yusuf Kagoma.

Esperance walirudisha mabao hayo kipindi cha pili, kabla ya kukosa mkwaju wa penalti ndani ya dakika tano za nyongeza baada ya zile 90 kumalizika.

Kwa matokeo hayo, ‘Wekundu wa Msimbazi’ wamebaki mkiani mwa Kundi hilo wakiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi nne.

Wakati huo huo, Stade Malien ya Mali iko kileleni ikiwa na pointi nane, ikifuatiwa na Esperance yenye sita, huku Petro Luanda ya Angola ikiwa nafasi ya tatu kwa zao pointi tano.

Ikizingatiwa kuwa ni timu mbili pekee za juu zitakazoingia hatua inayofuata ya robo fainali, ni wazi hesabu ni ngumu kwa ‘Wekundu wa Msimbazi’.

Katika mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa, Simba watafunga safari hadi Angola kuifuata Petro, kabla ya kurudi nyumbani kuivaa Malien.

Kwamba watalazimika kuifunga Petro ili kufikisha pointi nne, kisha kupata ushindi dhidi ya Malien, huku pia ikiombea wapinzani wake (Esperance na Petro) wasiongeze pointi katika mechi zao zijazo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img