8.4 C
New York

Mwanasiasa wa upinzani anusurika kuuawa

Published:

NAIROBI, Kenya

RIGATHI Gachagua, ambaye ni mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Kenya, amedai kuponea chupuchupu katika jaribio la kuuawa.

Kwa mujibu wa Gachagua, polisi walivamia kanisa alilokuwamo kwa ibada ya Jumapili ya wiki iliyopita mjini Othaya na kuanza kushambulia kwa risasi.

Gachagua alikuwa Makamu wa Rais wa Kenya, kabla ya ‘kutumbuliwa’ mwaka 2024, na tangu hapo amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali iliyoko madarakani.

Amekuwa akimtaja Rais William Ruto kuwa ni mtu anayesuka bila kuchoka mipango ya kumuua, japo kiongozi huyo hajawahi kumjibu.

Safari hii, licha ya kusema Ruto amehusika, Msemaji wa Serikali, Isaac Mwaura, amemjibu akisema Gachagua ndiye aliyetengeneza shambulizi hilo kama mtaji wa kisiasa.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha shambulizi hilo, ambalo hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img