TOKYO, Japan
HELIKOPTA iliyoripotiwa kubeba watalii wawili imepotea karibu na Mlima wa Aso nchini Japan. Ni moja ya milima yenye volkano hai nchini humo.
Taarifa ya polisi inaeleza kuwa helikopta hiyo iliondoka mjini Aso baada ya watalii kutembelea mbuga za wanyama lakini haikurudi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, pia taarifa ikithibitishwa na polisi, rubani wa helikopta hiyo aina ya Robinson R44 ni mwanaume mwenye umri wa miaka 64.
Akiwa na uzoefu wa miaka 40, alikuwa amebeba mwanamke na mwanaume, wote wakiwa ni raia wa Taiwan.
Inaelezwa kuwa helikopta hiyo iliyotengenezwa nchini Marekani ilikuwa katika safari yake ya tatu, kabla ya kupotea.
Hii si mara ya kwanza kwa Mlima Aso kuhusishwa na ajali za helikopta. Mwaka 2024, helikopta ililazimika kutua kwa dharura ikiwa eneo hilo, ambapo ilisababisha watu watatu kujeruhiwa.


