9.8 C
New York

Waziri Mkuu atangaza Uchaguzi New Zealand

Published:

WELLINGTON, New Zealand

WAZIRI Mkuu wa New Zealand, Christopher Luxon, ametangaza kuwa Uchaguzi Mkuu nchini humo utafanyika Novemba 7, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 21, 2026, Luxon amewataka raia wa New Zealand kuitumia nafasi hiyo kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.

Luxon, bosi wa zamani wa Shirika la Ndege, amekuwa kiongozi wa kwanza wa New Zealand kuchaguliwa kwa kura tangu utawala wa Jacinda Ardern.

Tangu alipoingia madarakani mwaka 2023, kumekuwapo na mwelekeo mzuri wa siasa za nchi hiyo, ingawa bado suala ya kudumaa kwa uchumi ni ‘pasua kichwa’.

Kwa sasa, wananchi wa New Zealander wanalalamikia kupanda kwa gharama za maisha, achilia mbali janga la uhaba wa ajira kwa kundi la vijana.

Serikali ya New Zealand inaundwa na muungano wa vyama vitatu vya siasa, ambavyo ni National Party cha Luxon, New Zealand First na ACT.

Akizungumzia mipango ya Chama chake kuelekea Uchaguzi wa Novemba, Luxon amesema kipaumbele chao kuwekeza nguvu nyingi katika ‘kufufua’ uchumi wa Taifa hilo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img