9.8 C
New York

AFCON … Salah na ‘mkosi’ wa kupishana na Kombe

Published:

RABAT, Morocco

USHINDI wa bao 1-0 waliopata Senegal dhidi ya Misri imeendeleza mkosi kwa Mohamed Salah katika ndoto yake ya kutwaa ubingwa wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).

Salah, licha ya mafanikio makubwa katika ngazi ya klabu akiwa na Liverpool, ubingwa wa AFCON umebaki kuwa ni ndoto isiyotimia kwa upande wake.

Akiwa na kikosi cha Misri, ambao ni mabingwa mara saba wa AFCON, amejikuta akiambulia patupu msimu huu wa mashindano hayo, ingawa alicheza kwa kiwango bora.

Katika fainali hizo zinazofanyika Morocco, Misri wametolewa wakati mchezaji huyo akiwa amefunga mabao manne na kutoa ‘asisti’ moja.

Kwa kulikosa msimu huu, sasa Salah atalazimika kusubiri hadi mwaka 2027, ambapo fainali za AFCON zitafanyika katika nchi tatu za Afrika Mashariki; Kenya, Uganda na Tanzania.

Wakati huo, atakuwa na umri wa miaka 35. Kama atakosa hapo, basi kuna uwezekano mkubwa wa Salah kustaafu akiwa hajawahi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Baada ya mabadiliko ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), fainali za AFCON sasa zitafanyika kila baada ya miaka minne, tofauti na miwili kama ilivyokuwa hapo awali.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img