YOUNDE, Cameroon
KIWANGO kibovu katika kipindi cha kwanza cha mchezo wao dhidi ya Morocco ndicho kilichoigharimu timu ya taifa ya Cameroon, kwa mujibu wa Bryan Mbeumo.
Straika huyo wa Manchester United alikuwa kikosini wakati timu yake ya taifa ya Cameroon ikifungwa mabao 2-0 na Morocco katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya AFCON 2025.
Mchezo huo uliochezwa Ijumaa ya Januari 9, 2026, katika Uwanja wa Mwanamfalme Moulay Abdellah mjini Rabat, uliishuhudia Morocco ikipata mabao yake kupitia kwa Brahim Diaz na Ismael Saibari.
“(Kipindi cha kwanza) Hatukucheza soka letu. Unaweza kuona tulivyoimarika zaidi kipindi cha pili, tuliwapa wakati mgumu kiasi,” amesema Mbeumo mwenye umri wa miaka 26.
Akicheza AFCON kwa mara ya kwanza tangu alipoamua kuiwakilisha Cameroon badala ya Ufaransa, Mbeumo hakufunga bao katika michuano hiyo, ingawa alitoa ‘asisti’ moja.


