10.7 C
New York

Arsenal yajitosa kwa Tyjon

Published:

LONDON, Uingereza

ARSENAL sasa imeingia mazima katika kuiwania saini ya kinda wa Blackburn Rovers, Igor Tyjon. Nyota huyo raia wa England ana umri wa miaka 17.

Hii si mara ya kwanza kwa Washika Bunduki hao wa London kuitaka saini yake. Walijaribu kumsajili mwaka jana lakini Blackburn walikataa ofa yao ya Pauni milioni moja.

Arsenal wanasaka mshambuliaji wa kati wa kuchukua nafasi ya ‘dogo’ Chido Obi aliyetimkia Manchester United mwaka jana.

Kwa taarifa zilizopo, Tyjon amegoma kusaini mkataba wake wa kwanza wa soka la kulipwa akiwa na Blackburn ya Championship (Ligi Daraja la Kwanza England).

Hatua yake ya kukataa kubaki imekuja baada ya kinda huyo kusikia saini yake inawindwa na Arsenal kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo barani Ulaya

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img