10.7 C
New York

Man City yavunja rekodi ya miaka 66

Published:

MANCHESTER, Uingereza

USHINDI wa mabao 10-1 dhidi ya Exeter City umeifanya Manchester City kuvunja rekodi ya Liverpool iliyodumu kwa miaka 66.

Man City ya kocha Pep Guardiola ilifanya maangamizi hayo jana Januari 10, 2026, katika mchezo wa Kombe la FA.

Kwa ushindi huo, Man City inakuwa timu ya kwanza katika historia ya soka la England kufinga mabao zaidi ya 10 ya mchezo mmoja tangu Liverpool ilipoifunga Tottenham mabao 13-2 mwaka 1960.

Wakati huo huo, straika mpya wa kikosi hicho, Antoine Semenyo, naye aliingia katika kitabu cha historia kupitia mchezo huo.

Semenyo alifunga bao moja na kutoa ‘asisti’, akiifikia rekodi ya mkongwe wa klabu hiyo, Sergio Aguero.
Nyota huyo raia wa Ghana, anakuwa mchezaji wa pili baada ya Aguero, kufunga na kutoa asisti katika mechi yake ya kwanza akiwa na ‘uzi’ wa Man City.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img