9.8 C
New York

Nigeria v Morocco … Diaz, Osimhen nani kupasuka nusu fainali?

Published:

RABAT, Morocco

WEKA kando nusu fainali ya Senegal na Misri. Nigeria dhidi ya Morocco ni vita nyingine kali ya kuisaka tiketi ya kuingia fainali msimu huu wa AFCON. Mechi itachezwa Jumatano ya Januari 14, 2025.

Nigeria ‘Super Eagles’ ilifika nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Algeria ya staa wa zamani wa Manchester City, Riyad Mahrez.

Super Eagles walipata ushindi mnono huo kupitia kwa mabao ya washambulia wake tishio kwa sasa, Victor Osimhen na Akor Adams.

Osimhen anayefanya vizuri barani Ulaya akiwa na Galatasaray, ameshafunga mabao manne msimu huu wa AFCON.

Wakati huo huo, wenyeji wa mashindano, Morocco ‘Simba wa Atlas’, wanajivunia kiwango bora cha mshambuliaji wao anayekipiga Real Madrid, Brahim Diaz.

Morocco waliitoa Cameroon katika hatua ya robo fainali, wakishinda mabao 2-0, huku Diaz akifunga bao moja na kufikisha matano msimu huu wa AFCON.

Mbali ya Diaz, pia safu ya ushambuliaji ya Morocco imekuwa ikipewa nguvu kubwa na beki wake wa pembeni, Achraf Hakimi.

Hisoria ya timu hizo katika michuano ya AFCON inaonesha kuwa Morocco na Nigeria zimekutana mara mbili, kila moja ikishinda mechi moja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img