9.3 C
New York

Marekani yaishambulia IS

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

VIKOSI vya Marekani vimeyashambulia yaliyotajwa na Rais Donald Trump kuwa ni makazi ya magaidi wa Kundi la IS nchini Syria.

Kwa mujibu wa Trump, wanajeshi wake wamelipiza kisasi kwa kile kilichofanywa na IS mwishoni mwa mwaka jana, ambapo wapiganaji wake waliua wanajeshi wawili wa Marekani.

“Ujumbe wetu uko wazi kabisa, kwamba kama utawaua wapiganaji wetu, basi tutakutafuta kokote pale duniani na kukuua. Haijalishi utajaribu kiasi gani kukimbia sheria,” amesema Trump.

Marekani na washirika wake wamefanya mashambulizi zaidi ya 35, ikielezwa pia kwamba ndege zaidi ya 20 zilihusika katika shambulizi hilo.

Taarifa zinataja ndege zilizotumika katika operesheni hiyo kuwa ni pamoja na F-15Es, A-10s, AC-130Js, MQ-9s na F-16.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img