9.8 C
New York

Ethiopia yaomba uenyeji AFCON 2028

Published:

ADIS ABABA, Ethiopia

SHIRIKISHO la Soka la Ethiopia (EFF) limetuma maombi ya kuziandaa fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2028.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limebadili mfumo wa michuano hiyo na sasa itafanyika kila baada ya miaka minne, tofauti na miwili kama ilivyozoeleka.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ratiba ya CAF, utaratibu huo mpya utaanza kutumikia kuanzia mwaka 2028.
Awali, Ethiopia ilitarajia kuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka 2029 lakini sasa imebadili uelekeo baada ya mabadiliko hayo ya CAF.

Licha ya Ethiopia kutokuwa na uwanja unaokidhi vigezo vya CAF, Serikali ya nchi hiyo inaamini kila kitu kitakwenda vizuri kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ya mwaka 2028.

Kuwa mwenyeji wa AFCON ni ndoto ya muda mrefu ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img