10.7 C
New York

Kiungo akubali mkataba mpya Liverpool

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

LIVERPOOL imefikia makubaliano na Dominik Szoboszlai, hivyo kiungo huyo atasaini mkataba mpya klabuni hapo.

Szoboszlai alitua Anfield mwaka 2023 baada ya kuonesha kiwango bora akiwa na wakali wa Bundesliga, RB Leipzig.

Chini ya kocha Jurgen Klopp, nyota huyo alicheza mechi 45 na kufunga mabao saba katika msimu wake wa kwanza Anfield.

Msimu wake wa pili, 2024-25, nao ulikuwa mzuri akiwa na kocha Arne Slot, ambapo alifunga mabao nane katika mechi 49, wakati timu hiyo ikichukua ubingwa wa Ligi Kuu.

Nyota huyo raia wa Hungary amekuwa wa moto pia msimu huu, akiingia kikosi cha kwanza mara sita na kuchangia mabao sita.

Kwa wiki za hivi karibuni, jina lake limekuwa likihusishwa na klabu kadhaa kubwa za Ulaya, zikiwamo Bayern Munich na Real Madrid.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img