10.7 C
New York

Ter Stegen ajiandaa kuondoka Barca

Published:

CATALUNYA, Hispania

MLINDA mlango wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen, atatimka klabuni hapo Januari hii, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Hispania.

Kipa huyo raia wa Ujerumani amejikuta kwenye wakati mgumu kurejea kikosini tangu alipopona majersha ya mgongo.

Kwa sasa, kocha Hansi Flick amekuwa akiwatumia zaidi Joan Garcia na Wojciech Szczesny, huku ter Stegen akiwa chaguo la tatu kikosini.

Hivyo, Ter Stegen anaangalia uwezekano wa kupata klabu itakayompa nafasi ya kucheza ili aweze kulishawishi benchi la ufundi la timu ya taifa ya Ujerumani.

Ikumbukwe, ni miezi takribani mitano pekee imebaki kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Tetesi zinaeleza kuwa huenda Ter Stegen akatimkia Girona kwa mkopo, ingawa klabu hiyo inaweza kuachana na biashara hiyo kutokana na mshahara wake mkubwa.

Barcelona wameitaka Girona kukubali kulipa asilimia 25 ya mshahara wake, jambo ambalo bado klabu hiyo haijakubaliana nalo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img