MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER City imefanikiwa kuinasa saini ya Antoine Semenyo na huenda straika huyo aliyetokea Bournemouth akaanza kuwatumikia matairi hao wa jijini Manchester wikiendi hii.
Kwa mujibu wa ratiba, Manchester City watashuka dimbani Jumamosi hii kumenyana na Exeter katika mchezo wa Kombe la FA.
Semenyo mwenye umri wa miaka 26, amejiunga na Manchester City kwa ada ya Pauni milioni 62.5, ambapo amesaini mkataba wa miaka mitano.
Mshambuliaji huyo raia wa Ghana, alikuwa mchezaji muhimu kwa Bournemouth na ameondoka akiwa amefunga mabao 32 na kutoa ‘asisti’ 13 katika mechi 110.
Ikumbukwe, Semenyo ndiye aliyefunga bao la la ushindi wakati Bournemouth ilipoifunga Tottenham mabao 3-2 katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Katika mahojiano yake baada ya kutambukishwa, Semenyo amesema ni ndoto iliyotimia kwake kujiunga na Manchester City na kufanya kazi chini ya Pep Guardiola.


