9.8 C
New York

Misri v Ivory Coast; Rekodi zimemaliza kazi mapema

Published:

RABAT, Morocco

TIMU ya soka ya taifa ya Ivory Coast, ambao ni mabingwa watetezi msimu huu wa fainali za AFCON, dhidi ya Misri inayoongoza kwa kulibeba taji la michuano hiyo. Patachimbika!

Kwa mujibu wa rekodi, Ivory Coast watashuka dimbani Jumamosi hii (Januari 10, 2026) wakiwa na tahadhari kubwa.

Ndiyo, wamefungwa mara saba na kushinda moja pekee katika mechi 11 walizokutana na Misri kwenye michuano hiyo.

Ivory Coast walijihakikishia nafasi ya kuingia robo fainali baada ya ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Burkina Faso.

Kwa upande wao, Mafarao wa Misri walivuka hatua iliyopita ya 16 Bora kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Benin katika mchezo uliofika dakika 120.

Kabla ya mechi hii, timu hizo zimeshawahi kukutana mara 21. Kati ya michezo hiyo, Misri imeshinda 11, imefungwa sita na kutoa sare mara nne.

Chini ya kocha mzawa, Hossam Hassan, Misri imefuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia na ubora wao unachangiwa na uwepo wa mastaa wake wawili wanaokipiga Ligi Kuu ya England, Omar Marmoush (Man City) na Mohamed Salah (Liverpool).

Kwa upande wao, bado Ivory Coast wako chini ya kocha Emerse Fae, ambaye ndiye aliyewapa taji la AFCON msimu uliopita.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img