11.6 C
New York

Cameroon v Morocco; Vita ya heshima, rekodi robo fainali AFCON 2025

Published:

RABAT, Morocco

NI kesho Januari 9, 2026, ambapo ni wazi mashabiki wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ watakuwa upande wa Cameroon katika mchezo dhidi ya Morocco.

Ndiyo, Stars ingeweza kufika robo fainali au zaidi ya hapo kama si penalti waliyonyimwa dakika za mwisho za mchezo wao na Morocco.

Ilikuwa ni mechi ya hatua ya 16 Bora, ambapo mwamuzi wa kati aligoma kuamua penalti, licha ya Iddy Suleiman ‘Nado’ kuangushwa kwenye boksi. Morocco ilishinda bao 1-0.

Bao pekee la vigogo hao lilifungwa na Brahim Diaz (dk. 64), akitumia ‘asisti’ ya nahodha wake anayekipiga PSG, Achraf Hakimi.

Sasa, Morocco ambao ni wenyeji wa fainali za AFCON watakutana na Cameroon katika mchezo wa robo fainali utakaochezwa kesho Januari 9, 2026, katika Uwanja wa Mwanamfalme Moulay Abdellah mjini Rabat.

Cameroon, mabingwa mara tano wa AFCON, waliingia robo fainali kwa kuifunga Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ mabao 2-1.

Morocco, licha ya mafanikio yake makubwa ya soka ya hivi karibuni, inafukuzia taji lake la kwanza la AFCON tangu ilipobeba mwaka 1976.

Kwa upande mwingine, rekodi zinaibeba pia Cameroon. Katika mechi tatu ilizokutana na Morocco kwenye michuano hii, Cameroon imeshinda tatu na kutoa sare moja.

Hata hivyo, kwa michuano yote, Morocco imeshinda mechi zote mbili ilizokutana na Cameroon hivi karibuni.
Vikosi: Cameroon – Epassy, Kotto, Tolo, Malone, Nagida, Namaso, Baleba, Ebong, Tchamadeu, Mbeumo na Kofane.

Morocco – Bounou, Hakimi, Aguerd, Masina, Mazraoui, El Khannouss, Al Aynaoui, Saibari, Díaz, Ezzalzouli na El Kaabi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img