9.8 C
New York

Robo fainali AFCON 2025; Mali, Senegal na ‘derby’ ya kibabe Morocco

Published:

RABAT, Morocco

NI ‘derby’ ya majirani wa Afrika ya Magharibi, ukiwa ni mchezo wa robo fainali ya michuano ya AFCON 2025 inayoendelea nchini Morocco.

Mali na Senegal zitakwaana kesho Januari 9, 2026, katika Uwanja wa Grand Stade de Tanger, mchezo utakaoamua timu ya kuingia nusu fainali.

Ikumbukwe, Mali walingia robo fainali baada ya ushindi wao wa penalti 3-2 dhidi ya Tunisia katika mchezo wa hatua ya 16 Bora.

Ni mchezo ambao Mali walibaki na wachezaji 10 tangu dakika ya 26 baada ya Woyo Coulibaly kulimwa kadi nyekundu kutokana na rafu aliyomchezea Hannibal Mejbri.

Ushindi dhidi ya Senegal utapeleka nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu walipofika hatua huyo mwaka 2013, ambapo walifungwa mabao 4-1 na Nigeria.

Senegal, kwa upande wao, walifanikiwa kuingia robo fainali wakipata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan.

‘Simba wa Teranga’ wako kwenye kiwango bora chini ya kocha mzawa, Pape Thiaw. Kikosi chake hakijafungwa katika mechi 15 za hivi karibuni; imeshinda 10 na sare tano.

Wakati huyo huo, Senegal wanabebwa na rekodi yao mbele ya Mali. Hawajafungwa katika mechi 10 zilizopita dhidi ya majirani zao hao.

Vikosi: Mali – Diarra, Dante, Camara, Diaby, Traore, Dieng, Bissouma, Coulibaly, Doumbia, Sangare na Sinayoko.

Senegal – Mendy, Jakobs, Niakhate, Koulibaly, Diatta, P. Gueye, I. Gueye, Diarra, Mane, Jackson na Ndiaye.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img