15 C
New York

Wakazi Venezuela wakimbilia madukani baada ya Maduro kukamatwa

Published:

CARACAS, Venezuela

 SAA chache baada ya Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, kukamatwa, Jumamosi Januari 3, 2026, na majeshi ya Marekani, wakazi wa mji mkuu Caracas walikimbilia madukani kununua chakula na mahitaji muhimu, huku mustakabali wa nchi hiyo ukiwa hauna uhakika.

Mbali na misururu mirefu ya watu katika maduka, video zilizopatikana mjini humo zinaonesha kuwa barabara nyingi za jiji hilo zilikuwa tupu na tulivu, hali inayoashiria hofu na taharuki miongoni mwa wananchi.

Makamu wa Rais wa Venezuela, Delcy Rodríguez, ametaka kuachiliwa mara moja kwa Rais Maduro na mke wake, Cilia Flores, akidai kuwa walivutwa kwa nguvu kutoka chumba chao cha kulala usiku wakati wa operesheni kubwa ya kijeshi iliyofanywa na Marekani.

Makamu wa Rais wa Venezuela, Delcy Rodríguez.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img