9.8 C
New York

Osimhen: Tumejipanga kuing’oa Msumbiji

Published:

RABAT, Morocco

STRAIKA wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Victor Osimhen, amesema wamejiandaa vizuri kwa mchezo wao wa Jumatatu ya wiki ijayo dhidi ya Msumbiji.

Timu hizo zitakwaana katika mtanange wa hatua ya 16 Bora ya msimu huu wa fainali za Mataifa Afrika (AFCON 2025).

Osimhen mwenye umri wa miaka 27, amecheza mechi zote tatu za hatua ya makundi, ikiwamo aliyovaa kitambaa cha unahodha walipoifunga Uganda mabao 3-1.

Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Msumbiji, nyota huyo amesema Super Eagles ni moja ya timu kubwa Afrika, hivyo kila mpinzani anapaswa kuhofia kukutana nayo.

“Ndiyo, nitaipa nchi yangu nafasi kubwa ya kupata ushindi. Sisi ni moja ya timu zinazoogopwa zaidi kwenye mashindano,” amesema mpachikaji mabao huyo wa Galatasaray ya Uturuki.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img