10.9 C
New York

AFCON yamponza Aubameyang, Serikali yamtimua

Published:

LIBREVILLE, Gabon

SERIKALI ya Gabon imetangaza kuvunja benchi la ufundi la timu ya soka ya taifa, ikiwa ni pamoja pia na kumtimua kikosini mshambuliaji wake, Pierre-Emerick Aubameyang.

Hatua hiyo ya Serikali kupita Wizara ya Michezo imekuja baada ya Gabon kufanya vibaya msimu huu wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025). Gabon wameishia hatua ya makundi, tena wakiwa wamefungwa mechi zote tatu na kumaliza mkiani mwa kundi lao.

Akizungumza baada ya kichapo cha mabao 3-2 katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Ivory Coast, Waziri wa Michezo, Simplice-Desire Mamboula, amesema:

“Kutokana na matokeo mabaya katika fainali za AFCON, Serikali imeamua kuvunja benchi la ufundi, kuifungia timu ya taifa mpaka pale itakapotangazwa, na kuwatoa kikosini wachezaji Bruno Ecuele Manga na Pierre-Emerick Aubameyang.

Chini ya kocha ambaye ni beki wa zamani wa timu hiyo, Thierry Mouyouma, Gabon ilikuwa Kundi F na timu za Cameroon, Msumbiji na Ivory Coast.

Katika michezo wa mwisho dhidi ya Ivory Coast, Gabon waliweza kutangulia kwa mabao 2-0, kabla ya wapinzani wao kusawazisha na kushinda mabao 3-2.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img