18 C
New York

EU wakanusha Ukraine kuishambulia Urusi

Published:

MOSCOW, Urusi

UMOJA wa Ulaya (EU) umekanusha madai ya Urusi iliyolalamikia ofisi zake za umma kushambuliwa na vikosi vya Ukraine.

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia mwandamizi wa EU, Kaja Kallas, Urusi inakuja na visingizio hivyo ili kuzorotesha jitihada za kumaliza vita kati ya nchi hizo.

Kallas ameibuka mitandaoni akisema hakuna ukweli kwamba ndege zisizo na rubani za Ukraine zilitaka pia kushambulia makazi ya Rais Vladmir Putin.

“Hakuna atakayekubaliana na uzushi wa wakandamizaji (Urusi) ambao wamekuwa wakishambulia miundombinu na raia wa Ukraine,” amesema Kallas.

Mapema wiki hii, Serikali ya Urusi iliibua madai kuwa Ukraine imelenga kushambulia nyumba ya Rais Putin huko Kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img