18 C
New York

Mahakama yataka Waziri Mkuu abaki gerezani

Published:

KUALA Lumpur, Malaysia

NI wazi sasa Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Najib Razak, ataendelea kusota gerezani baada ya Mahakama Kuu kukataa ombi lake la kutaka atumikie kifungo akiwa nyumbani.

Razak mwenye umri wa miaka 72, alihukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezani baada ya kashfa ya kuibiwa kwa Dola bilioni 4.5 katika Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali wa 1MDB.

Ni Mfuko ambao Razak aliuasisi mwenyewe mwaka 2009 kwa malengo ya kukuza maendeleo ya uchumi na uwekezaji. Lakini, mwanasiasa huyo alitajwa kuchota Dola milioni 9.9 katika Mfuko huo kwa matumizi binafsi.

Katika ombi lake, alitaka amalizie kifungo akiwa nyumbani, kwa kile kilichoelezwa na wanasheria weke kuwa ana changamoto ya kiafya.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img