10.2 C
New York

Gamondi katikati ya makocha 9 AFCON 2025

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

FAINALI za Mataifa ya Afrika za mwaka huu (AFCON 2025) zitakuwa na makocha 10 ambao itakuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hiyo wakiwa kwenye mabenchi ya ufundi.

Gamondi, kocha wa zamani wa Yanga, amechukua nafasi ya mzawa Hemed Suleiman ‘Morocco’ na hii ni mara ya kwanza kwa Muargentina huyo kuwa na timu ya taifa kwenye mashindano ya AFCON.

Pape Thiaw wa Senegal naye hii itakuwa mara yake ya kwanza kufanya kazi AFCON. Alichukua nafasi ya Aliou Cisse mwishoni mwa mwaka jana. Thiaw alitwaa taji la CHAN mwaka 2022.

Tangu alipopewa mikoba, Thiaw ameiongoza Senegal katika michezo 14, ambapo ameshinda 11, sare mbili na kufungwa moja (dhidi ya Brazil), huku timu hiyo ikifunga mabao 36 na kuruhusu sita pekee.

Kocha mwingine ambaye AFCON 2025 itakuwa mara yake ya kwanza ni Vladimir Petkovic wa Algeria. Raia huyo wa Uswis aliajiriwa mwaka 2023 akichukua nafasi ya Djamel Belmadi.

Ukiacha huyo, kuna kocha wa Misri, Hossam Hassan. Alicheza AFCON lakini fainali zijazo zitakuwa za kwanza kwake akiwa kocha. Ameshafanya kazi kubwa tangu alipoajiriwa, ikiwamo kuiwezesha Misri kufuzu fainali zijazo za za Kombe la Dunia.

Kwa upande mwingine, timu ya taifa ya Cameroon nayo ina kocha mgeni kwenye michuano ya AFCON 2025. Baada ya kumfuta kazi Marc Brys, kocha wa sasa ni David Pagou.

Ni kama ilivyo kwa Burkina Faso ambayo itakwenda AFCON 2025 ikiwa na Brama Traore. Gabon nayo ina kocha mgeni kwenye michuano hiyo, Thierry Mouyouma.

Si hao tu, bali pia Comoro ina Stefano Cusin, ambaye aliiwezesha timu ya taifa kufuzu fainali hizo ikiwa imedondosha pointi mbili tu kati ya 15. Vilevile, Zambia itakuwa na kocha mgeni, Moses Sichone, kama ilivyo kwa Morena Ramoreboli wa Botswana.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img