11.6 C
New York

Aubameyang kukosa ufunguzi AFCON 2025

Published:

MARSEILLE, Ufaransa

SHIRIKISHO la Soka la Gabon (FEGAFOOT) limethibitisha kuwa straika wa timu ya taifa hilo, Pierre-Emerick Aubameyang, atakosekana katika mchezo wao wa kwanza wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).

Gabon itaivaa Cameroon katika mchezo huo wa Kundi F utakaochezwa Desemba 24, mwaka huu, nchini Morocco.

Aubameyang atakosekana baada ya kupata majeraha ya paja wakati timu yake ya Marseille ilipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Monaco.

Katika mechi hiyo, mfungaji bora huyo wa muda wote wa Gabon aliumia zikiwa zimebaki dakika nne kabla ya mchezo huo wa Ligue 1 kumalizika.

“Baada ya mazungumzo na jopo la madaktari wa timu ya taifa na madaktari wa Olympique de Marseille, wamekubaliana kuwa atabaki Marseille kwa ajili ya matibabu,” wameeleza FEGAFOOT.

Kwa mujibu wa taarifa ya FEGAFOOT, nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 atarejea siku nne baadaye, wakati Gabon itakapoivaa Msumbiji.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img