11.6 C
New York

Mastaa wa kigeni Bongo watakaotua AFCON 2025

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

LIGI Kuu Bara imeendelea kuvuna ushawishi wake nje ya si tu Afrika Mashariki, bali pia katika soka la Afrika kwa ujumla.

Ni kutokana na ushawishi wake, sasa inashika nafasi ya tano katika zile Ligi Kuu bora zaidi Afrika, hiyo ikisababisha wachezaji wengi wa kigeni kutamani kuja kukipiga.

Safari hii, kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika, Ligi Kuu Bara itawakilishwa na mastaa kadhaa watakaokuwa na timu zao za taifa huko Morocco.

Djigui Diarra (Yanga, Mali)

Kipa huyo ni miongoni mwa wachezaji 28 waliojuhumishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Mali akiwa ndiye chaguo la kwanza langoni.

Diarra ameitwa kikosini, sambamba na makipa wengine wawili; Ismael Diawara (IK Sirius) na Mamadou Samassa (Laval).

Prince Dube (Yanga, Zimbabwe)

Kwa miaka mingi, Dube amekuwa mchezaji tegemeo kwenye safu ya ushambuliaji ya timu ya taifa ya Zimbabwe ‘The Warriors’.

Safari hii, ameingia tena katika orodha ya washambuliaji walioitwa katika kikosi kitakachokwenda Morocco kushiriki fainali za AFCON.

Amas Obasogie (Singida BS, Nigeria)

Kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ haijawahi kuwa rahisi. Ni kutokana na utajiri mkubwa wa vipaji vya soka nchini humo.

Hata hivyo, Obasogie wa Singida Black Stars ameitwa kutokana na uwezo wake mkubwa, akiunga na makipa wengine wawili; Stanley Nwabali (Chippa Utd) na Francis Uzoho(Omonia).

Khalid Aucho (Singida BS, Uganda)

Ukiacha Obasogie wa Super Eagles, Aucho ni mchezaji wa pili wa Singida Black Stars atakayeshiriki fainali za AFCON mwaka huu.

Aucho amejumuhishwa katika kikosi cha Uganda, akiwa sehemu ya nyota wa eneo la kiungo, kama ilivyo kwa Ronald Ssekiganda (APR FC), Bobosi Byaruhanga (Oakland Roots) na Baba Alhassan (FCSB).

Steven Mukwala (Simba, Uganda)

Staa huyo wa Simba naye atakwenda Morocco kushiriki fainali za AFCON akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’.

Ikumbukwe, ni katika kikosi chenye washambuliaji wa kiwango cha juu, akiwamo nyota tishio wa CS Sfaxien, Travis Mutyaba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img