11.6 C
New York

Simulizi za AFCON (5): Refa aliyemaliza mpira mara mbili

Published:

TUNIS, Tunisia

INAKUWAJE rahisi kulisahau jina la Janny Sikazwe katika historia ya michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON)? Ni ngumu.

Katika mechi ya hatua ya makundi kati ya Mali na Tunisia wakati wa fainali za mwaka 2022, jina la Sikazwe likawa gumzo katika mijadala ya soka ya ndani na nje ya Afrika.

Alifanya nini? Katika mchezo huo kati ya Mali na Tunisia, Sikazwe raia wa Zambia mwenye beji ya FIFA, aliwashangaza wengi alipopuliza kipenga cha mwisho katika dakika ya 85.

Hata baada ya kukumbushwa na mchezo kuendelea, Sikazwe alimaliza tena zikiwa hzijatimia dakika 90. Akawa kituko kweli kweli.

Hata baada ya jitihada za kurejesha mchezo ili dakika 90 zimalizike, wachezaji wa Morocco waligoma kurudi uwanjani. Mechi ikaishia hapo alipopata Sikazwe.

Baadaye, ilibainika kuwa mwamuzi huyo alipata changamoto ya afya wakati mchezo ukiwa unaendelea, hivyo kuathiri uwezo wake ndani ya uwanja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img