LOME, Togo
ILIKUWA ni mwaka 2010, ambapo kikundi cha watu wenye silaha za kivita kililiteka basi la wachezaji wa timu ya taifa ya Togo.
Ilikuwaje?
Ni fainali zilizofanyika Angola na tukio hilo lililoua watu watatu lilitokea mpakani mwa nchi hizo wakati wachezaji wa Togo wakiwa safarini kuelekea katika kituo chao cha mechi.
Straika wa Togo wakati huo, Thomas Dossevi, alisimulia tukio hilo akisema: “Tulishikiwa Bunduki, kama vile mbwa, tukiwa mpakani mwa Angola. Sijajua sababu.”
Baadaye, moja ya vikundi vya waasi kutoka katika Mji maarufu kwa utajiri wa mafuta nchini Togo, Cabinda, kilikiri kuhusika.
Katika tukio hilo, si tu watau waliofarikia, bali pia watu tisa, wakiwamo wachezaji, waliondoka na majeraha.
Aliyekuwa straika wa Arsenal wakati huo, Emmanuel Adebayor, alikuwa kwenye basi siku hiyo. “Wachezaji wote walikuwa wanalia, wengine walikuwa wakisali wakidhani siku ya kufa imefika.”
Licha ya baadhi ya wachezaji kutaka kucheza, agizo la Rais na Waziri Mkuu liliitaka timu hiyo kurejea nyumbani. Togo haikushiriki fainali hizo.



