15 C
New York

Aliyemuua Waziri Mkuu aomba radhi

Published:

TOKYO, Japan

TETSUYA Yamagami, ambaye ni mwanaume aliyekutwa na hatia katika mashitaka ya kumuua Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe, amekiri makosa na kuimba radhi familia ya mwanasiasa huyo.

Akiwa mbele ya Mahakama, Yamagami alisema anasikia vibaya kwa kile alichokifanya na sasa anaomba mke wa Abe, Akie, amsamehe. Yamagami alimuua Abe kwa kumpiga risasi katika tukio lililotokea Julai 8, 2022, huko Magharibi mwa Jiji la Nara. Abe alifariki akiwa anaendelea na matibabu.

Taarifa za kuuawa kwake zilizua gumzo duniani kote. Anakumbukwa kwa sera zake za kiuchumi, ambazo ziliifanya Japan kuwa na maendeleo makubwa, hasa katika sekta ya viwanda.

Akizungumza mahakamani, Yamagami alisema: “Nimeisababishia mateso makubwa ya miaka mitatu na nusu (familia ya Abe).”

Inaelezwa kuwa Yamagami amefichua sababu ya kumuua Abe kuwa ni kukerwa na hatua ya kiongozi huyo kushirikiana na Kanisa, ambalo anaamini lilitawaliwa na vitendo vya rushwa.

Kwa upande wake, mke wa Abe, Akie, ametumia mitandao ya kijamii kuandika: “Kumpoteza mume ni maumivu ambayo hayatapotea.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img