15 C
New York

Marekani yazitaka Thailand, Cambodia kumaliza vita

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

SERIKALI ya Marekani imezionya Thailand na Cambodia ikizitaka nchi jirani hizo kuacha mara moja vita inayoendelea. Kwa siku tatu mfululizo, yameshuhudiwa mapigano katika mpaka wa Thailand na Cambodia na kusababisha vifo vya watu takribani 10, huku wengi zaidi wakikimbia makazi yao.

Hii inakuwa mara ya pili kwa Marekani kuingilia kati mizozo huo, ambapo Oktoba, mwaka huu, Rais Donald Trump alizitaka nchi hizo kukaa mezani na kumaliza uhasimu wao.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani, Marco Rubio, Rais Trump angefanya mazungumzo ya simu na viongozi wa mataifa hayo.

Thailand na Cambodia zimekuwa kwenye mgogoro wa mpaka kwa miaka zaidi ya 100 sasa. Pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kusababisha mgogoro.

Takwimu za sasa zinaonesha kuwa uhasimu huo imesababisha watu zaidi ya 400,000 kukimbia makazi huko Thailand, huku 100,000 wakiripotiwa kwa upande wa Cambodia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img