11.6 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi A

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa mapema mwezi huu nchini Marekani. Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani. Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi A na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani.

Ni Kundi lenye Mexico, Afrika ya Kusini, Korea ya Kusini na timu moja itakayofuzu kupitia ‘playoff’ kati ya Czech, Denmark, Macedonia na Jamhuri ya Ireland.

Mechi ya ufunguzi ya Kundi hili ni kati ya Mexico na Afrika Kusini, ambazo pia zilifungua pazia na kutoka sare ya bao 1-1 wakati wa michuano ya mwaka 2010.

Mexico msimu huu inataka kuingia robo fainali kwa mara ya tatu, wakati Afrika Kusini chini ya kocha Hugo Broos inashiriki kwa mara ya kwanza tangu ilipokuwa mwenyeji miaka 15 iliyopita.

Korea Kusini nayo imo kwenye Kundi hili ikiwa ni mara yao ya 11 kushiriki Kombe la Dunia. Walifuzu bila kufungwa na itakumbukwa kuwa walifika nusu fainali walipokuwa wenyeji mwaka 2002.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img