Na Mwandishi Wetu, Gazetini
RAIS Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, wakijikita katika kudumisha ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa, kijamii pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa kwa kushirikiana na Marekani.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Desema 8, 2025, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma ambapo pande zote mbili zimeeleza nia ya kuimarisha na kupanua ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kuendeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuongeza fursa za ajira, huku Balozi Lentz akionyesha msukumo wa Marekani katika kushirikiana na Tanzania kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.






