11.9 C
New York

Kama huna NIDA, sahau kuhusu ndoa

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR

KWA ufupi, kama bado hujachukua kitambulisho chako, basi harakisha kwenda kwenye Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa [NIDA]. Kachukue sasa.

Na kama kadi uliyopewa awali imefutika au imechakaa, fika pale ofisini ili ubadilishiwe, huduma ambayo ni bure.

Kwanini unahitaji kitambulisho kipya? Ni kitambulisho kilichoboreshwa zaidi, tofauti na kile cha awali kilichokuwa na huduma nne tu. Kwa sasa, zimeongezeka nne, hivyo kitambulisho kimoja kinabeba taarifa za vitambulisho nane.

Kwamba ukiwa na kitambulisho cha sasa, hutolazimika kubeba cheti cha kuzaliwa, Bima ya afya, Leseni ya udereva, TIN namba (TRA), taarifa za Hali ya ndoa [umeoa/umeolewa], Kundi la damu, wala Hati ya kusafiria Afrika Mashariki na Kati [EAC].

Kubwa na muhimu zaidi, ili kufunga ndoa, utalazimika kuwa na kitambulisho cha NIDA, huku kila mtoto atakayezaliwa akipewa kitambulisho chake.

Wakati huo huo, kwa sasa kuna ‘NIDA Wallet App’, ambapo utakuwa na NIDA yako kwenye simu, hivyo kukupa uhuru wa ‘ku-scan’ na simu yako tu pale unapotaka kuthibitisha.

Aidha, vitambulisho vya zamani bado vinatumika lakini kwa wale wanaotumia namba tu, mwisho wake ni Februari, 2027. Kwamba ni baada ya miezi mitatu tu kutoka sasa.

Bado hujachelewa. Kwa sasa hivi kuna vitambulisho milioni 1.2 vimechapwa lakini watu hawajavichukua. Kama ulijiandikisha, nenda kavichukue Ofisi ya Wilaya ndani ya miezi mitatu.

Related articles

Recent articles