MERSEYSIDE, Uingereza
KOCHA wa Everton, David Moyes, ameungana na mashabiki wa timu hiyo akisema walikuwa sahihi kwa kile walichokifanya wakati wa mchezo wao wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bournemouth.
Mashabiki wa Everton walitumia dakika 90 za mchezo huo kupaza sauti za kupingana na taarifa za kuondoka kwa kiungo wao, Harrison Armstrong.
Armstrong ameonesha kiwango kizuri katika mechi zote 24 alizocheza Everton na alitumia dakika 87 katika mchezo dhidi ya Bournemouth.
Hasira za mashabiki zilitokana na taarifa zilizodai kuwa Nottingham Forest wamewasilisha ofa yao ya Pauni milioni 40 kwa ajili ya kinda huyo wa U-19 ya England.
Baada ya sare yao dhidi ya Bournemouth, Moyes alisema: “Nafikiri unapaswa kuwasilikiza mashabiki. Sio mara zote wanakuwa hawako sahihi.”
Hata hivyo, Moyes aliweka wazi kuwa wakati mwingine viongozi ndani ya klabu hulazimika kufanya maamuzi magumu kuisaidia timu.


