LONDON, Uingereza
WASHIKA Bunduki wa London, Arsenal, wameingia kwenye mazungumzo ya kumsajili staa wa Lille ya Ufaransa, Matias Fernandez-Pardo.
Licha ya Arsenal kuitaka saini yake, pia nyota huyo mwenye thamani ya Pauni milioni 60 anawindwa na matajiri wa klabu ya Newcastle United.
Fernandez-Pardo, kwa upande wake, anataka kuondoka Lille kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa kiangazi wiki ijayo.
Taarifa zinaeleza kuwa Arsenal wameona ni bora kumgeukia mshambuliaji huyo baada ya kuona imekuwa ngumu kumpata Julian Alvarez wa Atletico Madrid.
Uamuzi wa Arsenal kuachana na Alvarez raia wa Argentina umekuja baada ya nyota huyo kuonesha anataka kujiunga na Barcelona.


