23.5 C
New York

Grealish atakiwa Sunderland

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Sunderland imeanza kuiwinda saini ya winga wa kimataifa wa England, Jack Grealish, kwa mujibu wa mtandao wa Football Insider.

‘Black Cats’ wanaitaka saini ya nyota huyo kwa mkopo wakati huu akijiandaa kuondoka tena katika klabu yake ya Manchester City.

Grealish alimaliza msimu uliopita akiwa kwa mkopo Everton baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha Pep Guardiola.

Kocha wa sasa, Enzo Maresca, amempa nafasi mara kadhaa lakini mabosi wa Man City bado wanapiga hesabu za kumtoa kwa mkopo.

Man City, kwa upande wao, wako tayari kumwachia endapo klabu inayomtaka itakubali kulipa sehemu ya mshahara wake wa Pauni 300,000 kwa wiki.

Related articles

Recent articles