21.4 C
New York

Olise avunja rekodi ya Pele

Published:

MIAMI, Marekani

MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Ufaransa, Michael Olise, ameivunja rekodi ya mkongwe wa Brazil, Pele.

Nyota huyo wa Bayern Munich ameandika historia mpya, licha ya Ufaransa kufungwa mabao 6-4 katika mchezo wa jana Julai 18, 2026, wa kusaka mshindi wa tatu msimu huu wa Kombe la Dunia.

Olise amefikisha asisti saba katika michuano ya mwaka huu, akimpiku Pele aliyetoa sita katika mashindano ya mwaka 1970.

Kati ya asisti zake saba, tano ametoa kwa nahodha wake wa kikosi, Kylian Mbappe. 

Hata hivyo, Olise amemaliza fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu akiwa hajafunga bao.

Related articles

Recent articles