37.6 C
New York

Wanafunzi 36 bado wanashikiliwa na watekaji

Published:

LAGOS, Nigeria

WANAFUNZI 36, pamoja na mfanyakazi wa shule, bao hawajaachiwa na kikundi cha waasi, kwa mujibu wa Polisi nchini Nigeria.

Mapema wiki hii, waasi hao wakiwa na silaha waliwateka wanafunzi na mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Serikali iliyoko mjini Lassa, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Jumatatu, wakati wanafunzi hao wakiwa kwenye mtihani.

Polisi wamethibitisha kufanikiwa kuokoa wanafunzi nane, lakini wamekiri kuwa wengine 36 wamebaki mikononi mwa watekaji.

Kati ya waliobaki, 25 ni wavulana, 11 ni wasichana, achilia mbali mfanyakazi wa shule hiyo.

Related articles

Recent articles