MADRID, Hispania
REAL Madrid wako kwenye hatua nzuri ya kukamilisha dili la lejendari wa Manchester City, Bernardo Silva, akitarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Jose Mourinho.
Taarifa zinaeleza kuwa Mreno huyo ameshakubali mkataba wa miaka miwili kujiunga na Madrid na dili litatangazwa siku chache zijazo.
Hivi karibuni, Madrid walitangaza kumrejesha Mourinho, ikiwa ni miaka 13 tangu alipoondoka klabuni hapo. Amesaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Benfica ya Ureno.
Silva (31), aliondoka Man City akiwa mchezaji huru baada ya kumalizika kwa msimu wa 2025-26. Ni baada ya miaka tisa ya kuitumikia klabu hiyo, akiipa mataji makubwa 20, yakiwamo sita ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa.
Hizo zinaweza kuwa habari mbaya kwa Barcelona na Atletico Madrid, ambazo pia zilikuwa zikijaribu kuinasa huduma ya ‘mido’ huyo.


