MUNICH, Ujerumani
KLABU ya Bayern Munich inaamini itafanikisha mpango wake wa kuinasa huduma ya kiungo wa pembeni wa Manchester United aliyemaliza mkopo wake Barcelona, Marcus Rashford.
Wakati huo huo, ripoti zinaeleza kuwa Man United hawatamrejesha kikosini, na badala yake wako tayari kusikiliza ofa itakayofika mezani.
Bayern wako kwenye mazungumzo na wawakilishi wa nyota huyo, ikielezwa kuwa tayari wametanguliza ofa yao ya euro milioni 25.
Rashford (28), alikuwa kwenye kiwango bora akiwa kwa mkopo Barcelona, ambapo alimaliza msimu wa 2025-26 akiwa amefunga mabao 14 na kutoa asisti 14.
Msimu huo, pia aliiwezesha Barcelona kutwaa mataji makubwa mawili ya ndani; Ligi Kuu (La Liga) na Supercopa de Espana.


