MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER City itauanza msimu ujao (2026-27) bila kocha raia wa Hispania, Pep Guardiola. Enzo Maresca aliyewahi kuinoa Chelsea ndiye atakayekuwa kwenye benchi la ufundi.
Wakati ikiendelea kuhusishwa na wachezaji wapya, nyota walio mlangoni kuondoka Etihad ni Rodri, Savinho na Jack Grealish aliyemaliza msimu uliopita akiwa Everton.
Wakati huo huo, winga wa Kibrazil, Savinho, huenda akatimkia Tottenham kwa Pauni milioni 50, huku Nico Gonzalez na Tijjani Reijnders nao wakihusishwa na mpango wa kuondoka.
Ni kama ilivyo kwa mabeki Nathan Ake na Rico Lewis, kiungo Kalvin Philips, pamoja na kipa chaguo la pili kikosini, James Trafford.
Aidha, Man City haiko tayari kumwachia beki wake anayewindwa na Bayern Munich, Josko Gvardiol, kama ilivyo kwa kipa namba moja raia wa Italia, Gianluigi Donnarumma.


