25.9 C
New York

Usajili dirisha kubwa Ulaya: Nani aondoke, nani abaki? – ARSENAL

Published:

LONDON, Uingereza

BAADA ya ubingwa wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya England tangu mwaka 2004, Arsenal wataingia msimu ujao wa 2026-27 wakiwa mabingwa watetezi.

Pia, watataka kutimiza ndoto ya ubingwa wa Ligi ya Mabingwa baada ya kufungwa na PSG katika mechi ya fainali msimu wa 2025-26.

Katika kusuka upya kikosi, kocha Mikel Arteta amewafungulia mlango wa kutokea kipa Karl Hein na mabeki Jakub Kiwior na Joshua Nichols.

Nyota wengine wanaohusishwa na mlango wa kutokea Emirates ni Martin Odegaard, Ethan Nwaneri, Ben White, Leandro Trossard na Gabriel Martinelli.

Kwa mujibu wa ripoti, wanaohusishwa na nafasi ya beki wa kati anayocheza White ni Ivan Fresneda na Tino Livramento.

Arteta amewataka mabosi kumsajili winga wa AC Milan, Rafael Leao, wakati huo pia akihusishwa na mastaa wa PSG, Bradley Barcola na Khvicha Kvaratskhelia.

Pia, Washika Bunduki wamekuwa wakiripotiwa kuwafukuzuia Morgan Gibbs-White (Nottingham Forest) na Morgan Rogers (Aston Villa).

Related articles

Recent articles