18.4 C
New York

Antonio Conte avunjiwa mkataba Napoli

Published:

MILAN, Italia

KLABU ya Napoli imetangaza kuachana na kocha wake, Antonio Conte, akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.

Mwaka mmoja uliopita, Conte aliyewahi kuzinoa Inter Milan, Chelsea na Tottenham aliipa Napoli taji la Ligi Kuu (Serie A).

Msimu huu wa 2025-26 uliomalizika hivi karibuni, Napoli ilimaliza katika nafasi ya pili ikiwa imeachwa pointi 11 na mabingwa Inter Milan.

“Tungependa kumshukuru kocha na wasaidizi wake kwa kazi yao nzuri. Tunawatakia kila la kheri katika changamoto yao mpya,” imeeleza taarifa ya Napoli.

Baada ya kuachana na Napoli, Conte anahusishwa na mpango wa kurudi kwenye benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Italia aliyowahi kuinoa kuanzia mwaka 2014 hadi 2016.

Related articles

Recent articles